Tuesday , 16th Feb , 2016

Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika linalohusika na biashara za rejareja NRF, imesema kuwa Marekani imetumia kiasi cha dola bilioni 20 kwenye sikukuu ya wapendanao.

Baadi ya rais wanaoishi nchini Marekani wakiwa katika Chakula cha Pamoja cha Usiku.

Taarifa hiyo inasema kuwa kiasi hicho cha fedha kimetumika kununulia vyakula,maua pamoja na vito huku ikieleza kuwa zaidi ya watu 7,300 wameshiriki kwenye sherehe hiyo kwa kununua bidhaa mbalimbali pamoja na kufanya sherehe.

Katika sikukuu hiyo kila raia wa nchi hiyo ilikadiriwa kutumiwa wastani wa dola za Kimarekani 144.84 sawa na ongezeko la asilimia 3.2 kulinganisha na mwaka jana.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika hilo asilimia 38 walisheherekea kula chakula cha jioni katika migahawa mbalimbnali ambapo walitumia wastani wa dola bilioni 4.5 huku nusu ya wamarekani walinunua kadi kwa wastani wa dola bilioni 1.1

Pia tafiti hizo zimesema kuwa dola bilioni 4.4 zimetumika katika manunuzi ya vito vya thamani,dola bilioni 2 katika mavazi huku bilioni 1.9 kwenye manunuzi ya maua.