Saturday , 30th Jan , 2016

Nyota wa muziki Mandojo amesema kuwa, kwa mwaka huu ameamua kupiga hatua tofauti katika muziki wake ambapo atatoka na solo project, tofauti na utaratibu wao wa siku zote wa kufanya ngoma pamoja kama Mandojo na Domokaya.

Mandojo

Mandojo ameieleza eNewz kuwa, hatua hiyo haimaanishi kuwa wametengana kimuziki kutokana na wao kuwa ni kitu kimoja , akiwa sasa katika kukamilisha kazi yake mpya, hapa akiwa ananyoosha maelezo kuhusiana na mpango huo.

Mandojo amesema kuwa, kazi yake ya kufungulia mwaka ameifanya chini ya studio ya Kiri Records, mtayarishaji akiwa ni Rash Don, akimshirikisha msanii mkali wa miondoko ya Dancehall nchini, Chibwa.