Tuesday , 26th Jan , 2016

Klabu ya Simba SC imesema inaamini itachukua ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara msimu huu kutokana na maboresho yaliyo ndani ya kikosi hicho.

Afisa habari wa Simba SC Haji Manara amesema, wanaingia katika mzunguko wa pili wakiwa na mawazo ya kuibuka mabingwa wa ligi hiyo kwani mpaka sasa wamezidiwa pointi sita na wapinzani wao ambao ni Yanga ambayo ni sawa na michezo miwili na wao wanamichezo 15 ambayo wanaamini wataweza kuzifikia na kuwazidi na hatimaye kuchukua ubingwa huo.

Manara amesema, uongozi mzima, benchi la ufundi na wachezaji lengo lao kwa sasa ni kuchukua ubingwa japo wanaamini ligi ni ngumu na hakuna mechi nyepesi lakini marekebisho yaliyo ndani ya kikosi hicho yatafanikisha kufikia lengo.