Monday , 25th Jan , 2016

Wamiliki wote nchini waliokabidhiwa viwanda vya serikali baada ya kubinafsishwa lakini wakashindwa kuviendeleza wamepewa hadi Julai wawe wameanza uzalishaji vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage baada ya kutembelea na kukagua viwanda vya serikali vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji mkoani Morogoro.

Waziri Mwijage amemwagiza Mkurugenzi wa Viwanda wa wizara hiyo kufuatilia wizara ya fedha na mipango, taratibu mbalimbali za kisheria kwa wamilki wa viwanda vilivyofungwa ama kushindwa kuendeleza uzalishaji kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.

Aidha Mwijage amesema lengo la serikali ni kuona viwanda vyote vilivyobinafsishwa na kushindwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa vinafanya kazi za uzalishaji kulingana na maelekezo yaliyomo ndani ya mikataba ili kuwawezesha kutoa ajira nyingi kwa watanzania.