Thursday , 14th Jan , 2016

Mamlaka ya Bandari Tanga inakabiliwa na changamoto ya chombo cha kuingiza meli bandarini kiitwacho maarufu kama tagi hali inayopelekea kukwama kwa huduma muhimu katika bandari hiyo.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Henry Arika akizungumza na Waandishi wa Habar

Akizungumza Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Henry Arika amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza kuwa kusuasua kwa matengenezo ya kifaa hicho ni kutokana na tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuzuia vibali kwa wafanyakazi wote wa serikali kusafiri nje ya nchi hali ambayo sasa inawalazimu kukodi kifaa kutoka katika bandari ya Mombasa.

Amesema matumizi ya kifaa hicho katika bandari ya Tanga yalisitishwa na mafundi wa mamlaka hiyo kuwa kifaa hicho hakiwezi kutumika tena mpaka kifanyiwe matengenezo.

Baada ya kusikia maelezeo hayo ndipo mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akasema swala hilo atalifikisha kwa Waziri Makame Mbarawa ili alifanyie kazi.