Damas Lukungu amesema, kwa mwezi huu mashindano hayo yatafanyika Januari 30 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo washiriki vilakuwa vilabu vya Mkoa wa Dar es salaam, Taasisi na Shule za msingi na Sekondari pamoja na mikoa ambayo inaalikwa lakini itajigharamia katika ushiriki wa michuano hiyo.
Lukungu amesema, mashindano hayo ni yawazi yakiwa na lengo la kutafuta Timu ambayo itaweza kushiriki mashindano ya Taifa ambayo hufanyika kila mwaka yakiwa na lengo la kutafuta timu ya Taifa itakayoweza kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya nje ya nchi.