Wednesday , 6th Jan , 2016

Kaya 1500 hazina makazi katika kata ya Magomeni wilayani Kilosa Mkoani Morogogo baada ya nyumba zao zaidi ya 250 kubomoka na nyingine 500 kujaa maji baada ya mvua kunyesha kwa saa nne na kusababisha mafuriko katika kata hiyo.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Magomeni , Mjini Kilosa wakipita kwenye barabara iliyojaa maji ya mafuriko ya mvua pamoja na mizingo mikononi na vichwani

Wananchi hao walioathirika na Mafuriko hayo wakiongea kwa uchungu wameitupia lawama serikali kwa kuahidi kujenga matuta katika mto Mkondoa ili kupunguza kasi ya Maji katika mto Mkondoa.

Akizungumza na Waandishi wa habari Diwani wa kata hiyo Bw, Abdallah Ahueni ameiomba serikali kuwasaidia makazi pamoja na chakula kutokana na hasara kubwa waliyoipata wananchi hao ikiwemo kuharibiwa kwa vyakula vyao.

Kwa upande wake Mbunge wa Vitu Maalumu Mkoa wa Morogoro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Devotha Minja ameitupia lawa serikali kuhusiana na Ujenzi wa tuta hilo huku akiwataka wananchi waliokuwa katika nyumba hatarishi kuhama wakati viongozi hao wakitafuta njia ya kuwasaidia.