Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene
Akizungumza katika mafunzo hayo, afisa elimu kutoka idara ya usimamizi wa elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dodoma, Hellen Msellem, ambaye pia ni mratibu wa mafunzo hayo, amesema mafunzo hayo yamewekwa mahususi kwa ajili ya kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo hayo ambayo katika miaka mitatu iliyopita wanafunzi walionekana kuto fanya vizuri.
Amesema, kutokana na mwaka huu kiwango cha ufaulu kuwa ni asilimia 80, imewekwa mikakati itakayowawezesha walimu na wanafunzi kufikia malengo, ambapo miongoni mwake ni pamoja na huo wa kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu ili na wao waende kuwafundisha walimu wengine.
Aidha, baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo, wameiomba serikali kuto ishia katika masomo hayo manne pekee, isipokuwa mpango huo uendelee katika masomo mengine kwani kwa kufanya ivyo itasaidia kwa kiasi kukubwa kuondoa tatizo la kufeli kwa wanafunzi wengi hapa nchini.