Wednesday , 16th Dec , 2015

Serikali imesema itawanyang'anya viwanja wamiliki wote wa viwanja waliopewa kwa ajili ya kuviendeleza na kuwekeza kwa shughuli za kimaendeleo ambapo ndani ya miaka mitatu wakiwa hawajafanya chochote katika maeneo.

Mheshimiwa Angelina Mabula Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Akizungumza na East Africa radio Naibu Waziri Wizara ya Ardhi ,Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula amesema serikali itaanza ukaguzi wa maeneo yote ya viwanja ambayo watu wamepewa muda mrefu lakini hawajawekeza mpaka sasa.

Mh. Mabula amesema wataangalia muda wa mtu aliepewa kiwanja na kitu gani alitaka kuwekeza na kitu gani na eneo hilo kwa muda wa sasa linatumika kwa shughuli gani na kama ameenda kinyume na makubaliani Serikali itamnyang'anya.

Aidha Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kuwa Wananchi ambao wanahodhi maeneo makubwa kwa ajili ya kujipatia pesa kinyume na taratibu ambapo wanapewa kwa ajili ya uendelezaji wa maeneo waliyopewa.