Tuesday , 15th Dec , 2015

Serikali imeombwa kuanzisha mfuko maalum kwa ajili kutoa mikopo kwa vyama vya ushirika wa akiba na mikopo nchini hatua ambayo imetajwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mitaji kwa vyama hivyo katika kuwakopesha wajasiliamali wadogo.

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini mhe. Vedastus Mathayo

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini mhe. Vedastus Mathayo,akiwashauri wajasiliamali katika manispaa hiyo kutumia vema fedha zamikopo wanayoipata katika kuinua hali zao kiuchumi.

Nao baadhi ya wajasiliamali wa Imara Saccos, wamesema elimu na ushirikiano ndiyo nguzo kuu ya kuwawezesha kufanya biashara zao kwa faida zaidi katika kupambana na umasikini miongoni mwao.

katika mkutano huo wa wajasilimali mbunge huyo wa jimbo la Musoma mjini ametoa ahadi ya kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa Saccos na vikundi ambavyo tayari vimesajiriwa huku akikabidhi shilingi milioni tatu kwa ushirika huo wa imara saccos.