D'Banj
Msanii huyu amesisitiza kuwaa muda sahihi ukifika, atatangaza harusi yake kama ambavyo imekuwa kwa mastaa wengine Nigeria na sehemu nyingine.
D'Banj ambaye amekuwa akihusishwa na stori za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo Kenya Moore, na mwigizaji Genevieve Nnaji, amesema kuwa, taarifa zote hizi si za kweli na yupo katika mpango wa kuchukua hatua za kisheria kwa wazushi wa habari hizi.
D'Banj amesisitiza kuwa, anaonelea ni busara kwa suala zima la yeye na mpenzi aliyenaye sasa kubaki kuwa ni mambo binafsi mpaka pale atakapooa rasmi, siku na tarehe ambayo haijulikani.