Kamanda wa polisi Mkoani Geita,Loston Mponjoli Lwabulambo
Katika tukio hilo waliouawa kutokana na tukio hilo lililotokea kijijini hapo ni pamoja na mtotoMasanyiwa Malongo mwenye umri wa miezi minane aliyeuawa pamoja na mama yake Sophia Silyvester(40).
Wengine waliouawa katika tukio hilo ni Mariam Lusafisha (48) pamoja na mama yake mzazi Shinje Honera(80) wote wakazi wa kijijini humo na aliyejeruhiwa katika tukio hilo ni Malongo Dutu(46) ambaye alijeruhiwa sehemu ya mbele yakichwa na kusababisha kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa ajili ya matibabu.
Kamanda wa polisi Mkoani Geita, Mponjoli Lwabulambo, alithibitisha kuwepo kwa tukio na kwamba ufafanuzi wake utatolewa kwa waandishi wa habari baadaye hii leo huku akisema upepelezi wa kutafuta wahusika unaendelea.
Naye Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita, Dkt. Ndalo Ndalo, alisema alipokea majeruhi mmoja wa tukio hilo jana saa 12 alfajiri, ambapo alitibiwa kisha kuruhusiwa kuondoka kutokana na hali yake kuonekana ya kuridhisha.
'' Malongo Dutu, tumempokea akiwa na jeraha la kukatwa na panga kichwani sehemu ya mbele ambapo alilazwa wodi namba nane, lakini baada ya matibabu tumemruhusu kuondoka kutokana na hali yake kuendelea vizuri.''alisema Dakitari Ndalo.
Wakizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo baadhi ya wananchi wamedai wakati tukio hilo linatokea ndugu hao walikuwa nje wakiota moto baada ya chakula cha na ndipo walifika watu wawili waliopiga hodi na baada ya muda waliwaweka chini ya ulinzi kisha kuanza kuwakata mapanga.
Inadaiwa huenda chanzo cha mauaji hayo kimetokana na imani za uchawi ikiwa ni siku chache tu tangu kutokea kifo cha Samweli Nane ambaye alikuwa mume wa Mariam aliyefariki kutokana na kusumbuliwa na kifua.
Habari zinasema Nane aliyefariki Novemba 12, mwaka huu alikuwa akiwatokea ndugu zake mara kwa mara hali iliyosababisha waamini kuwa huenda kifo chake kilitokana na imani za uchawi.
Wamedai katika tukio hilo kikongwe aliyeuawa alikuwa akiishi kijiji cha Kishinda na alifika hapo baada ya msiba wa mkwewe huyo na kabla ya kuondoka yaani kuamalizia matanga ndipo ukatili huo wakutisha ulipotokea na yeye kuwa mmoja wa waliouawa kIkatili.