Marehemu Alex Ssempijja aliyecheza kwenye video ya wimbo wake Eddy Kenzo 'Sitya Loss'
Mwanamuziki Eddy Kenzo aliyeimba ngoma ya 'Sitya Loss' amethibitisha kifo cha dansa huyo mtoto, Alex Ssempijja, anayetokea eneo la Katwe, ambaye amekufa kwa ajali ya baiskeli usiku wa jana Jijini Kampala.
Dogo Ssempijja pia alicheza katika video za nyimbo nyingine za Eddy Kenzo katika ngoma kama Mundeke Numbe, Sitya Loss, Jambole, Zivuga pamoja na So Good.
Video ya ngoma ya Sitya Loss sio tu iliwavutia wapenzi wa muziki bali pia ilimpatia Eddy Kenzo tuzo wa BET.
Rest in Peace Alex Ssempijja, gone too soon and so young.