Tuesday , 1st Apr , 2014

Kundi la muziki la Mafikizolo ambalo Jumamosi hii litadondosha burudani kali jijini Dar es Salaam, limeweza kuteka vichwa vya habari tena hasa baada ya kung'ara kwa kutokea katika tuzo kubwa za muziki za Afrika Kusini- SAMA za mwaka huu.

Mafikizolo

Mafikizolo ambao tayari wana rekodi ya kushinda katika tuzo mbalimbali, katika Tuzo hizi wanapambana na wasanii wengine wakali kuwania tuzo ya Albam Ya Mwaka kupitia albam ya Reunited, Kundi La Mwaka, Kolabo Bora ya Mwaka, na Albam Bora ya Pop ya Mwaka.

Sherehe za ugawaji wa tuzo hizi zitafanyika huko Afrika Kusini tarehe 28 mwezi huu, lakini kabla ya hapo, habari kubwa ni kuwa Jumamosi hii Mafikizolo watakuwa Live Jijini Dar es Salaam wakimwaga burudani yenye viwango pale katika ukumbi wa Mlimani City. Hii sio ya kukosa kabisaaa.