Saturday , 14th Nov , 2015

Muongoza video ambaye pia ni Rapper na muimbaji Jae Baz ambaye jina lake halisi anaitwa Joseph Obaruyi Edo Ehigie ni moja kati ya Waongoza video na Ma-Rapper wazuri walioko nje

ambao wameweza kufanya kazi nyingi na zenye ubora licha ya kutofahamika na watu wengi kwa sasa hapa Afrika Mashariki.

Rapper Jae Baz ameshapanda jukwaa moja na wasanii wakubwa kama 2pistols, T-Pain, 9Ice, 2Face, Majek Fashek, Timaya, Flavour N'abania, P Square, Wiz Kid, Yvonne Chaka Chaka na KK Fosu.

Jae Baz amezaliwa mwaka 1988 na amewahi kuishi Italia, Marekani ila makazi yake kwa sasa ni nchini Canada ambako anafanya shughuli zake za muziki na pia yeye ni CEO wa Corporations na mwanzilishi wa A Supreme Land-Lord Muziki ambaoo yeye na wenzake wanaongoza video za muziki, wanatengeza filamu, wanatengeneza matangazo tofauti na mambo mengine ya burudani.

Rapper Jae Baz amewahi kutoa nyimbo kadhaa ambazo zilivuma kidogo kwa watu wanaomfatilia wanajua ninachozungumzia hapa na wanamfahamu vizuri katika uwezo wake wa kuchana na kutembea na beat

Wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Endelessy ‘ ndio wimbo wake ambao ameachia video ya wimbo huo na imeongozwa na jamaa waitwao Alpha na Pictures jamaa wanafanya naye kazi katika kampuni yao ya kuongoza filamu na matangazo

“Nimewahi kufanya nyimbo nyingi huko nyuma na pia nimeongoza video kadhaa huko nyuma naamini kuna watu wananifahamu ambao walikuwa wanafatilia muziki wangu. Kwasasa nimeachia video ya wimbo wangu uitwao ‘Endelessy’ kwakweli ni video nzuri sana na nimeonesha uwezo wangu mkubwa katika wimbo huo. ..naomba watu watembelee you tube na waangalie tv stations mbalimbali pia wataweza kuuona”.Alisema Jae Baz

Tazama baadhi ya nyimbo zake hapa

Watch "Jae Baz - Shake It Down" on YouTube - https://youtu.be/jlklut7nZwE

Watch "Our Pain/Our Hustle Is Peace (Official Music Video) - Jae Baz" on YouTube - https://youtu.be/G0ZVO4a5ijI

Watch "UnOfficial Release - Ebe Nō Rhien Rhien [Endlessly] Jae Baz ft. ADO" on YouTube - https://youtu.be/eU8C3m6RJkw