Tuesday , 10th Nov , 2015

Wakati Uganda inaelekea kuanza mbio za kampeni za uchaguzi mkuu mapema mwakani, staa wa muziki Eddy Kenzo ametajwa kuwa star wa kwanza mkubwa kuungana na mgombea wa urais wa upinzani Amama Mbabazi kumsapoti katika kampeni zake.

Eddy Kenzo

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo hazijatoka rasmi, Kenzo yupo katika nafasi ya kujitengenezea shilingi milioni 100 za Uganda kwa ajili ya kumtengenezea mgombea huyo nyimbo na pia kuzunguka naye katika mikutano yake ya kampeni.

Kwa upande wa chama tawala, licha ya Rais Museveni kupata sapoti ya moja kwa moja kutoka kwa wasanii wakubwa kama Chameleone, Juliana na wengineo, binafsi ameamua kuingia studio kutengeneza wimbo wa kusifu mafanikio ya chama chake kama mkakati wa kuvuta wapiga kura kumpatia nafasi nyingine kuiongoza Uganda.