Tuesday , 10th Nov , 2015

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa bodi hiyo haitatoa mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016 na kusema kuwa taarifa hizo si za kweli .

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw, George Nyatega

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Bw, George Nyatega na kuongeza kuwa taarifa sahihi ni kwamba hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836 wa mwaka wa kwanza.

Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo na katika awamu ya Pili iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji 28,554 wamepangiwa mikopo.

Taarifa hiyo inasema kuwa lengo la lodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830, wanapata mikopo.

Aidha, bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.