Monday , 2nd Nov , 2015

Chama cha ADC kupitia kwa Mwenyekiti wake Said Miraji kimesema kuwa mgogoro Zanzibar unasababishwa na ubovu wa katiba ya sasa ya Zanzibar ambapo amezitaka pande mbili zenye mgogoro kutatua suala hilo kidiplomasia.

Mwenyekiti wa chama cha ADC Said Miraji Abdallah

Aidha Miraji ameongeza kuwa Uchaguzi huo hauwezi kurudiwa chini ya tume ambayo imekiri udhaifu wa kusimamia uchaguzi hivyo inapaswa kuwajibika na kutoka nafasi kwa Rais kuteua wajumbe wengine wa tume hiyo ndipo uchaguzi ufanyike.

Miraji ameongeza kuwa tume iliyotoa mapungufu katika ufanyaji kazi haistahili kuandaa uchaguzi mwingine na kusema kuwa suala la tume hiyo kuchukua maamuzi ambayo hayawezi kuhojiwa sehemu yoyote ni tatizo la kupata viongozi visiwani humo.

Aidha amesema kuwa endapo hatua za haraka zisipochukuliwa kutatua tatizo hilo hali ya kiusalama katika visiwa hivyo ipo mashakani kutokana na mgogoro huo ambao unaonekana kuwa tishio la Usalama wa Wanzabar.

Hali ya kiuchumi Zanzibar imeanza kutetereka baada ya wafanyabaishara kutoka Tanzania kugoma kupelekea biashara zao visiwani humo kama vile vyakula, na mbogamboga.