Saturday , 31st Oct , 2015

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania NEC Jaji Damian Lubuva ametoa shukrani zake kwa watanzania ambao walijitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wao katika uchaguzi mkuu nchini uliofanyika Oktoba 25.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania NEC Jaji Damian Lubuva ametoa shukrani zake kwa watanzania ambao walijitokeza kwa wingi kuchagua viongozi wao katika uchaguzi mkuu nchini uliofanyika Oktoba 25.

Jaji Lubuva aliyetoa kauli hiyo jana wakati wa kukabidhi vyeti kwa washindi wa uchaguzi huo Dkt John Pombe Magufuli ambaye ameteuliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Samiah Suluhu Hassan ambaye ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

Jaji Lubuva alisema watanzania walijitokeza kwa wingi kupiga kura ambapo jumla wa watu milioni 15.5 walipiga kura ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo ni wapiga kura milioni 8.3 walijitokeza kupiga kura na kuwapongeza wanainchi kwa jinsi walivyopiga kura kwa utulivu.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameipongeza Tanzania kwa ajili kuendesha uchaguzi wa amani na hatimaye mgombea Dkt John Magufuli kushinda uchaguzi huo.

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu amewapongeza watanzania, serikali na vyama vya siasa nchini kwa kuendesha uchaguzi wa amani ulioandaliwa vizuri na kufanyika Oktoba 25.

Taarifa hiyo imemalizia kwa kusema kwamba kitendo cha wananchi wa Tanzania cha kuwajibika na kupiga kura na kusubiri matokeo bila vurugu kilionesha ukomavu wa kidemokrasia amani na utulivu.