Wednesday , 21st Oct , 2015

Nyota wa muziki Barnaba Classic aliyepata ugeni mzito wa staa wa muziki Jose Chameleone katika studio yake ya High Table siku ya jana, ameeleza mashabiki wake kuwa ziara hiyo imefungua milango, ikiwa ni matayarisho ya projectz nzito na Chameleone.

Nyota wa muziki nchini Tanzania Barnaba Classic

Barnaba ameeleza kuwa, amekuwa na wakati wa manufaa sana na msanii huyo wa kimataifa, sambamba na kufanya kazi pamoja ambayo inakwenda kwa jina Nakutunza itakayotoka mwezi ujao kama ambavyo anaeleza mwenyewe hapa.