Friday , 16th Oct , 2015

Serikali imesema thamani ya bidhaa za Tanzania zilizopelekwa Rwanda imekuwa na kufikia shilingi milioni 196.4 kutoka mwaka jana huku ubora wa bidhaa za Tanzania katika soko la Afrika Mashariki umetajwa kuongezeka.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwani Wema

Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema amesema hayo wakati akizungumzia maonesho ya nguvukazi yanayofahamika kama jua kali,yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 8 mwaka huu.

Wema amesema kuwa madhumini ya maonyesho hayo ni kuwezesha Urasimishaji kwa shughuli za sekta hiyo rasmi katika ukanda wa Afrika mashariki kwa kuwapatia fursa wajasiriamali kuonesha ubunifu wa bidhaa na kukuza masoko.

Ameongeza kuwa maonesho hayo ni ya 16 ambapo idadi ya wajasiriamali wanaoshiriki imeongezeka kutoka 41 mwaka 199 hadi kutarajiwa wajasiriamali 1000 mwaka huu.

Wema amesema maonesho hayo ya nguvu kazi au Jua kali yamesaidia kuobreha bidhaa za Tanzania ambapo kwa kipindi hca mwaka 2014 Tanzania ilitoa mshindi wa kwanza wa teknolojia ya Mawasiliano.