Wednesday , 14th Oct , 2015

Kada wa siku nyingi wa chama cha Mapinduzi CCM,tangu mwaka 1967, Balozi Juma Mwapachu ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kutokana na kile alichoeleza kuwa ni CCM kupoteza lengo la kuwa chama cha watu.

Kada wa siku nyingi wa chama cha Mapinduzi CCM,tangu mwaka 1967, Balozi Juma Mwapachu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana Jijini Dar es Salaam Balozi Mwapachu amesema dalili za CCM, kuwa chama cha viongozi wachache zilianza siku nyingi hasa katika kipindi cha uongozi wa Jakaya Kikwete.

Balozi Mwapachu amesema kuanzia hii leo amejivua uanachama rasimi na kuongeza kuwa amechagua siku ya leo kwa kuwa ndio siku mwafaka ambayo inahusu uanasiasa wake tangu mwaka 1967.

Amesema moja ya sababu nyingine zilizomfanya kuhama chama hcake hicho ni kutoakana na kukiukwa kwa mchakato wa uchaguzi wa uteuzi was urais mjini Dodoma na yeye alionyesha msimamo wake dhahiri kumuunga mkono Mh. Edward Lowassa.

Mwapachu ameongeza kuwa uamuzi wake wa kuumuunga mkono Lowassa sio wa kukurupuka bali ni kutokana na kumfahamu mgombea huyo ambae kwa sasa anagombea kupitia CHADEMA, tangu mwaka 1990 kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo pamoja na majukumu ya kichama.

Amemsifu Lowassa kuwa amejaliwa nuru na uwezo wa kuongoza na kupendwa na watu na msikivu na ni kiongozi asiependa ukiritimba na utovu wa nidhamu iwe kwa upande wa watumishi au wananchi wenyewe.