Monday , 12th Oct , 2015

Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa kutumia ushawishi wao kuwahimiza wanachama wao kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Jaji Mutungi ameyasema leo jijin Dar es salaam na kusisitiza kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi hivyo ni muhimu kudumisha Amani iliyopo kwani machafuko yakitokea hayatabagua na wote tutaathirika.

Jaji Mutungi ameongeza kuwa dhamana ya nchii hii ipo mikononi mwa viongozi wa vyama vya siasa kwani wana wafuasi wengi ambao huwasikiliza na kuwaamini.

Aidha msajili huyo wa vyama amewaasa waandishi wa habari kutumia kalamu zao vyema kwa kuhubiri amani na upendo na kuepuka kuandika habari za uchochezi na wawasaidie watanzania kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia katika kufanya uchaguzi wa amani.