Konshens
Ujio wa msanii huyu ni moja ya matukio makubwa kabisa katika historia ya burudani nchini Kenya, akiwa bado anafanya vizuri kabisa na ngoma kali kama vile Bounce, Walk n Wine, Gal a Bubble na nyinginezo.
Kwa upande mwingine, staa mwingine mkali wa Kimataifa wa miondoko ya Reggae, Gramps Morgan naye ametangaza kuwa, yupo tayari kabisa kwa ajili ya kufanya ziara kubwa Afrika, ambapo miongoni mwa nchi anazotazamia kuzifikia kwa burudani, Kenya vilevile Tanzania zinatokea kwenye orodha.