Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Celestine amesema, katika ufunguzi wa michuano hiyo katika mechi zilizochezwa Jumamosi na Jumapili kiujumla waliona kila kitu kilikuwa kama walivyopanga.
Mwesigwa amesema, ripoti itasaidia kuweza kujua mambo yaliyokuwa yakitokea ambayo kwa upande wao hawakuyaona hivyo kwa masaa 48 wanaamini watapata ripoti na kupitia kwa ajili ya kujua muenendo wa ligi hiyo.



