
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema kuwa wamefurahishwa mno kwa vilabu hivyo toka nje ya Dar es salaam hasa Ndanda FC ambayo inatokea mkoani Mtwara kwakufanikiwa kupanda kwa mara ya kwanza kupanda ligi hiyo na hivyo kutoa fulsa kwa wanamtwara kuona tena ligi kuu kwa mara nyingine baada ya miaka mingi kupita tangu timu kipenzi cha wanamtwara kushuka Daraja wakati huo
Kitendo cha timu hiyo kupanda kutatanua wigo wa ligi hiyo mikoani kwani timu nyingi zimekua zikitoka jijini Dar es salaam na hivyo kuwanyima fulsa mashabiki wa mikoa mingine kuona soka la ligi kuu kwahiyo sasa Ndanda imewapa fulsa hiyo kutokana na umoja wa wanamtwara wakiongozwa na serikali ya mkoa huo.
