Mkurugenzi wa mtandao wa watetezi wa haki za binadam (THRDC) Onesmo Olengurumwa.
Akiongea na waandishi wa habari amesema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona sheria imeanza kufanya kazi wakati baadhi ya vipengele havijafanyiwa marekebisho.
Aidha amebainisha kuwa endapo mahakama itapuuzia malalamiko yao watakata rufaa mpaka pale watakapoona wamesikilizwa.
Mnamo Septemba mosi, serikali kupitia wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ilitangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria ya Makosa ya Kimtandao(Cyber Crime Law) ambapo wadau mbalimbali waliitolea maoni tofauti wengine wakisema itasaidia huku wengine wakipinga wakisema itabana uhuru wa habari.