Thursday , 27th Mar , 2014

Idara ya wagonjwa na afya ya akili katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili nchini Tanzania inakabiliwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa wa akili kutokana na hospitali za Manispaa za Jiji kutokuwa na huduma hizo.

Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya taifa Muhimbili Dkt Maria Njelekela.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dkt. Frank Aloyce Masao amesema huwa wanapokea wagonjwa wa akili wa kulazwa kati ya 3 na 5 kwa siku hali inayosababisha wagonjwa kujaa wodini na kufikia asilimia 150 na 250 kwa baadhi ya wodi kila siku katika Hospitali ya Muhimbili.

Dkt. Masao amesema katika hospitali hiyo wana upungufu wa wafanyakazi 144 wa kada mbalimbali wanaohitajika ili kukidhi mahitaji ya idara ya kijiji cha marekebisho ya akili kinachojulikana kama Vikuruti ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa kada ya wanasaikolojia .