Monday , 31st Aug , 2015

Rapa wa nchini Kenya, CMB Prezzo amezikonga nyoyo za wengi baada ya kuasili mtoto wa kiume kutoka kituo cha watoto cha Grace Community Children’s Home na kumtambulisha kwa dunia kama mwanaye ambaye anatambulika sasa kama Gabriel Prezzo.

staa wa muziki wa nchini Kenya Prezzo akiwa na mtoto aliyemuasili na kumbatiza jina Gabriel Prezzo

Prezzo ametaka mashabiki wake kutambua kuwa mwanae huyo ni mwanachama mpya wa kundi lake la CMB, hatua ambayo imempatia pongezi nyingi kutoka kwa wapenzi wa sanaa yake, akiwa tayari anafahamika kuwa ni baba wa mtoto mmoja wa kike.

Hatua hii ya Prezzo inakuwa ni sawa na ile ya msanii wa muziki Bahati kutoka nchini Kenya, ambaye naye aliasili mtoto mwishoni mwa mwaka jana.