Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Dkt. Jakaya Kikwete
Akifungua Kikao cha Halmashauri kuu jana Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa idadi kubwa ya watu waliojitokeza kugombea uongozi ndani ya chama hicho inaonyesha kuwa chama hicho kina mvuto mkubwa.
Kikao hicho ambacho kina kazi ya kupitia uteuzi wa majina ya wagombea wa ubunge na uwakilishi katika majimbo.
Kikwete amefungua Mkutano huo baada ya kuelezwa na katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kuwa wajumbe waliohudhuria walikuwa 362 kati ya wajumbe 374 waliotarajiwa ambao ni sawa na asilimia 96 ya wajumbe wote.
Rais Kikwete amesema kazi ya wajumbe hao ilipunguzwa na vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati Kuu ambavyo vilikutana na kuchambua majina na sifa za wagombea hivyo akaeleza kuwa kazi iliyobakia kwa Halmashauri Kuu si kubwa sana.