Friday , 31st Jul , 2015

Staa wa muziki Ray C, baada ya kuwa anapata maombi zaidi ya 500 kila siku kufuatia hatua yake ya kutangaza kutafuta mume katika mtandao, ameiambia eNewz kuwa suala hilo lilikuwa ni utani tu na kwa yeye kufikia kuamua kuolewa bado sana.

msanii wa miondoko ya bongofleva Ray C

Tangazo hili la Ray C ambalo limemvuta hata Staa wa muziki wa Kenya, Ringtone kutafuta mawasiliano ya mwanadada huyo kwa njia ya mtandao, limemfanya Ray C kwa mara nyingine kuweka bayana si kweli anatafuta mume, akikanusha kuumiza hisia za watu waliomchukulia serious akiamini kuwa mume mwema anatoka kwa Mungu. .

Vilevile Ray C akazungumzia upande wa gemu ya muziki na kuweka wazi kuwa, amepanga kurejea rasmi baada ya kumaliza dozi ya Methadone mwezi wa 9 mwaka huu katika kuondokana na uathirika wa matumizi ya dawa za kulevya.