Friday , 31st Jul , 2015

Mwanadada aliyewahi kufanya vizuri katika chati za muziki Afrika Mashariki, Chantelle pamoja na mumewe J Blessings, wamepatwa na pigo kubwa hasa baada ya kufiwa na mtoto wao wakiume, Kylie aliyekuwa na umri wa miezi 7 tu.

staa wa muziki wa nchini Kenya Chantelle akiwa na mtoto wake

Kufuatia taarifa hizo za kuhuzunisha, salamu za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali zimeendelea kumiminikia familia hii, huku maswali yakiwa mengi juu ya sababu hasa zilizopelekea kifo cha mtoto huyo ambaye alikuwa faraja kubwa kwa familia hiyo.

Bado hakuna maelezo rasmi juu ya kile ambacho kimesababisha kifo cha mtoto huyo, baba yake mzazi J Blessings akielezea kwa kifupi juu ya pigo na huzuni kubwa kwao kutokana na kifo cha mtoto wao.