Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo katika moja ya vikao vya kamati kuu
Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete atastaafu baada ya uchaguzi huo akiwa amemaliza muhula wake wa pili na wa mwisho madarakani, kwa mujibu wa Katiba.
Maafisa wa ngazi ya juu wa chama hicho watawachagua wagombe watatu, ambao hatimae watapigiwa kura katika mkutano mkuu Julai12 kumpata mgombea Urais.
Miongoni mwa wanasiasa wanaotajwa zaidi ni Makamu wa Rais Mohamed Gharib Bilal, Waziri mkuu Mizengo Pinda, Jaji mstaafu Agustino Ramadhani, Waziri wa mambo ya nchi za nje Benard Membe na Waziri mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Pia katika orodha ya wagombea 39 yumo waziri wa sheria aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro.