Monday , 29th Jun , 2015

Serikali imesema kwamba kuimarishwa kwa sera za mazingira ya uwekezaji duniani kupewe kipaumbele katika kuimarisha sekta hiyo Tanzania, Afrika na dunia nzima kwa ujumla.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji Mhandisi Christopher Chiza

Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji Mhandisi Christopher Chiza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Dunia ya uwekezaji 2015 uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kwa mwaka 2014 uwekezaji duniani ulipungua kwa asilimia 16 kufikia Dola trilioni 1.2 za Marekani kutokana na kuyumba kwa uchumi wa sera zisizo thabiti kwa mataifa mengine.

Aidha ripoti hiyo inaonyesha kuwa mitaji ya uwekezaji katika nchi zinazoendelea ulifikia kiwango cha Dola bilioni 681 hiyo ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.

Kwa sasa uchumi wa nchi zinazoendelea unavutia mitaji ya uwekezaji duniani kwa asilimia 55 na kati ya nchi kumi zinazovutia uwekezaji kwa wingi duniani tano zinatoka katika nchi zinazoendelea.