Friday , 26th Jun , 2015

Maadhimisho ya siku ya dawa za kulevya duniani leo hii yamefanyika kwa harakati mbalimbali za kuongeza uelewa na vilevile kupambana na janga hili, huku bado ikionekana kuwa uelewa wa tatizo hili bado haujapewa uzito unaostahili,

Ray C

Maoni hayo yametolewa na Ray C, star wa muziki ambaye bado anaendelea na matibabu kutoka katika tatizo la matumizi ya dawa hizo.

Ray C kutokana na uzoefu ambao ameutoa kutoka shughuli zake mbalimbali kuokoa waathirika wengine, amesema kuwa siku hii ni muhimu sana, na kufunguka kwao kwa sehemu kunaendelea kusaidia tatizo hili kuendelea kueleweka ukubwa wake, akilitambua kama janga kama ilivyo kwa gonjwa la UKIMWI.