Monday , 22nd Jun , 2015

Mshambuliaji mpya wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Khalfan Ngassa leo amerejea kwa muda katika timu yake, Yanga SC na kufanya nayo mazoezi.

Kwa upande wake Ngassa amesema, alipewa ruhusa ya kuja kuchezea timu ya taifa, bahati mbaya siku mbili kabla ya mechi na Uganda, akaambiwa hawezi kucheza kwa hivyo wakati wa kusubiri ameamua kufanya mazoezi Yanga kujiweka fiti wakati anasubiri tiketi ya kurejea Afrika Kusini na hata hivyo Yanga ni timu yake na hajaondoka kwa ubaya na anaweza kurudi wakati wowote.

Ngassa alisaini FS Mei mwaka huu Mkataba wa miaka minne baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC akiiacha na ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.