Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani wakati wa uzinduzi wa baraza la Wafanyakazi wa Sektretarieti ya Ajira.
Bi. Celina amesema kuwa kumekuwepo na changamto nyingi zilizokuwa zinaukabili mfumo wa zamani wa utumaji maombi ikiwemo kuchelewa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya waombaji, uhaba wa fedha na pamoja na udanganyifu wa vyeti.
Amesema kuanza kutumika kwa mfumo huo kutatatua changamto hizo hasa kutokana na mfumo huo wa barua ulikua unalalamikiwa na wadau wengi kuwa una upendeleo katika chaguzi zake.
Naye Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nchini Xavier Daudi amesema waliamua kubuni njia mbadala ya kutuma maombi kutokana na kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu wanaotuma maombi katika taasisi hiyo.