
Akizungumza bungeni Mjini Dodoma, Rage amesema, huu ni wakati wa Serikali kumtimua kocha huyo kwa kuwa ameshindwa kusimamia na kuipa mafanikio timu hiyo ambapo kocha huyo hana uwezo wa kuifundisha timu hiyo zaidi ya kupoteza muda na kufaidi mshahara mnono anaolipwa na Serikali.
Stars imepata matokeo mabaya katika mchezo wake wa awali wa kuwania kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika AFCON 2017 na kupelekea Tanzania kuburuza mkia katika kundi G ambalo lina timu za Nigeria, Misri na Chad.
Nooij ameiongoza stars katika mechi 18 na kati ya mechi hizo ameshinda mechi tatu pekee