Tuesday , 9th Jun , 2015

Serikali ya Tanzania imekiri kuwepo kwa tatizo la watumishi wa afya katika maeneo mbalimbali nchini hivyo kuzorotesha utoaji huduma za afya kwa wagonjwa.

Akijibu swali bungeni leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Mhe. Hawa Ghasia, amesema tatizo la kukosekana kwa watumishi wa afya limetokana na uhaba wa watumishi hao katika soko la ajira akitolea mfano wilaya ya Kilwa ambayo inauhitaji wa watumishi 1,275 ambapo mpaka sasa watumishi waliopo ni 275 pekee.

Aidha Waziri Ghasia amesema kuwa serikali kwa kutambua changamoto hiyo wameanzisha mikakati ikiwemo kuhakikisha kuwa kuwa kunakuwepo na watumishi wakutosha kwa kuweka vivutio kwa watumishi na kuongeza udahili wanaojiunga katika fani ya afya ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wanafunzi kuchukua masomo ya sayansi.

Akitaja baadhi ya vipaumbele vilivyowekwa ni pamoja na kuanzisha mifumo ya mikataba ya kufanya kazi kabla hawajaamua kuacha kazi kugawa upya watumishi waliopo katika ngazi ya wlaya na mikoa ili kutoa kipaumbele katika maeneo yenye uhitaji.