Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake Shilole aka 'Shishi Baby'
Nuh ameileza eNewz kuwa, yeye pamoja na Shilole wanapenda sana kupata mtoto wao, ila anafahamu kuwa hiyo ni mipango ya Mungu na wakati wowote kutoka sasa ikitokea baraka hiyo watafurahi, huku akiweka mipango ya ndoa baada ya kutambulishana kwa wazazi.