Sunday , 7th Jun , 2015

Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe, Mtanzania, Mbwana Samatta amesema hatoongeza mkataba katika Klabu yake ya Tp Mzembe kwani anataka kufika mbali zaidi katika soka.

Akizungumza na East Africa Radio, Samatta ambaye yupo na stars kambini Adis Ababa nchini Ethiopia, amesema, zimekuja ofa nyingi zilizopelekea yeye kutokuongeza mkataba.

Samatta amesema, mipango ya kwenda nchi za Ulaya kucheza soka ipo na ndoto zake zinakaribia kutimia na hata kwa upande wa bosi wa Tp Mazembe amekuwa mgumu na hata sasa ni m,gumu kumpa ushirikiano katika hilo suala lakini kama bosi wake ataendelea kutompa ushirikiano angependa kuondoka akiwa huru mkataba wake ukimalizika.

Samatta amesema ni vilabu mbalimbali vinavyohitaji huduma yake ambavyo wakala wake amemueleza ambavyo ni kutoka nchi za Ufaransa, Ubeligiji na Ureno lakini kwa upande wake anapenda kuanzia Ufaransa au Ubeligiji ili iwe rahisi kwake kuingia nchi za Ulaya kutokana na ligi za nchi hiyo kutokuwa na ushindani mkubwa.