
Afisa habari wa shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, muamuzi msaidizi namba moja atatoka nchini Angola huku namba mbili akitokae nchini Elitrea ambapo wa akiba atatoka nchini Zambia huku kamishna wa mchezo huo akitokea nchini Rwanda.
Lucas amesema, katika mchezo huo kutakuwa na Mratibu mkuu wa mashindano ambaye atawasili nchini akitokea nchini Msumbiji.
Lucas amesema, mchezo huo utakuwa na changamoto kubwa kutokana na matokeo ya Yanga aliyoanza nayo dhidi ya Mo Bejaia ambapo alifungwa bao 1-0.
Lucas amesema, wamefanbya tathimini ya matokeo na wanaamini Yanga bado inanafasi ya kufanya vizuri kwani katika hatua waliyofikia Yanga bado wanamechi za marudiano na katika hatua ya makundi zinahitajika timu mbili ili ziweze kusonga mbele.
Kikosi cha Yanga tayari kimewasili mjini Antalya, Uturuki kwa kambi ya siku tano kujiandaa na mchezo wake wa pili wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, ambapo yanga inatarajiwa kuwasili nchini Juni 25.