Tuesday , 7th Jun , 2016

Klabu ya Yanga imewanasa Kipa wa Tanzania Prisons aliyekuwa akitakiwa na Klabu ya Simba Benno Kakolanya na beki wa Mtibwa Sugar Andrew Vincent 'Dante'.

Aliyekuwa kipa wa Prisons ambaye sasa ni Kipa wa Yanga, Beno David Kakolanya

Benno na Dante wote wamesaini miaka miwili kuwatumikia mabingw ahao wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Dante sasa anakwenda kugombea namba dhidi ya mabeki wengine wa kati wa Yanga, Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro', Kevin Yondan, Pato Ngonyani na Vincent Bossou.

Kwa upande wa Mlinda mlango Kakolanya anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco ma kufanya idadi ya makipa wane ndani ya klabu hiyo.

Hata hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya.