
Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini
Taarifa ya Yanga iliyotolewa leo mchana inafuta uvumi ulionea kuwa baadhi ya wachezaji hawakuhudhuria mazoezi ya jana na leo kwasababu za maslahi.
''Kikosi kimeendelea na mazoezi yake kwenye uwanja wa Police Kurasini uku kikiwakosa wachezaji ambao wapo kwenye kambi ya timu taifa, wale wa u23 pamoja na wachezaji watatu Juma Mahadhi, Pappy Tshishimbi na Baruan Akilimali ambao bado ni majeruhi'', imeeleza taarifa hiyo.
Jana iliripotiwa kuwa baadhi ya wachezaji wa Yanga wameshindwa kufika mazoezini hivyo kuonekana kwa wachezaji hao hii leo kumeweka sawa suala hilo.
Katika mchezo wa mwisho wa Yanga kwenye ligi kuu ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.