Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Wachezaji 26 wa timu ya Dar es salaam Young Africans maarufu kama Yanga ya jijini Dar es salaam nchini Tanzania wanatarajia kuanza rasmi mazoezi hapo kesho chini ya kocha msaidizi Juma Pondamali mara baada ya kutangazwa kusajiliwa kuitumikia klabu hiyo msimu huu.
Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema wachezaji walioachwa ni 11 ambao wamemaliza mikataba yao na kubaki na wachezaji 26 ambao wanatarajia kuendelea nao msimu huu.
Amesema bado wanaendelea na taratibu za usajili wa wachezaji wengine ambao watawahitaji na wanatarajia kutangaza mara watakapokamilisha zoezi la usajili wa wachezaji hao.
Aidha Kiziguto amesema kuhusu kocha wao mpya Masio Maximo anatarajia kuwasili mwishoni mwa Juma lijalo ambapo ataungana na timu hiyo ambayo hivi sasa ipo chini ya kocha Juma Pondamali





