
Kikosi cha Lipuli FC
Akiongea na www.eatv.tv msemaji wa Lipuli FC Clement Sanga amesema tayari wameshaombana radhi kwa matokeo ya jana hivyo kwasasa akili zao zote wamezielekeza kwenye mchezo ujao dhidi ya African Lyon.
''Kwasasa timu bado ipo jijini Dar es salaam tukijiandaa na mchezo wetu dhidi ya African Lyon na kuhusu mchezo wa jana makosa ya mchezaji wetu Paul Ngalema yalitugharimu na kupelekea kufungwa na ndivyo ulivyo mchezo wa soka, hayo yamepita radhi na tumewaomba radhi mashabiki'', amesema.
Sanga amebainisha kuwa kocha wa timu hiyo Suleiman Matola ametoa mapumziko ya siku moja kwa wachezaji ambayo ni leo hivyo kesho watarejea mazoezini tayari kwa kujiandaa na mechi ya Ijumaa dhidi ya African Lyon.
Lipuli FC sasa ipo katika nafasi ya 13 ikiwa na alama 12 kwenye mechi 11. African Lyon ipo kwenye nafasi 18 ikiwa na alama 8 katika mechi 12. Jana Lipuli FC ilifungwa bao 1-0 na Yanga.