Friday , 1st May , 2015

Young Africans kesho inatarajia kushuka dimbani nchini Tunisia katika mchezo wake wa marudiano ya kombe la shirikisho barani Afrika hatua ya 16 bora dhidi ya Etoile du Sahel ya nchini Tunisia dimba la Olympique de Sousse katika mji wa Sousse.

Katika taarifa yake, kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema wana ari ya kushinda mechi hiyo licha ya kuwaacha wachezaji wake tegemezi katika msafara wao wa Tunisia.

Katika mechi iliyochezwa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, Yanga ililazimishwa sare ya 1-1 hivyo kuwa na kibarua kigumu cha kushinda ugenini huku wenyeji wao wakililia suluhu ili kucheza hatua inayofuata ambapo timu itakayoibuka na ushindi itaingia hatua ya mtoano kabla ya hatua ya nane bora katika michuano hiyo.