Saturday , 9th Jun , 2018

Wizara ya Michezo nchini Ghana imekivunja chama cha soka baada ya Rais wake kunaswa katika video akionekana akipokea Pesa kinyume na utaratibu.

Kwesi Nyantakyi alipigwa picha akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi habari mpekuzi aliyejifanya kuwa mfanyibiashara aliye na hamu kubwa kuwekeza katika soka Ghana.

Mustapha Abdul-Hamid, waziri wa habari Ghana amesema serikali imeamua kuchukua hatua za mara moja kukivunja chama cha soka Ghana GFA huku mtuhumiwa akiwa hajapewa nafasi ya kujieleza.

Waziri huyo amesema hatua za muda za kuongoza soka Ghana zitatangazwa hivi karibuni, huku kukisubiriwa kuundwa chama kipya.