Akizungumza na East Africa Radio, mmoja wa wachezaji wa mchezo huo, Moureen Sizya amesema wanawake wasiweke mawazo kuwa mchezo huu ni wa wanaume pekee, lakini hata wanawake wanauwezo wa kucheza na kufanya vizuri zaidi tofauti na wanavyofikiria.
Moureen amesema wazazi pia wanatakiwa kuwapa nafasi watoto wakike kuweza kushiriki katika michezo mbalimbali hususani mpira wa kikapu ambao unazidi kukosa wachezaji wa kike hapa nchini.