
Wanariadha hao wamejiunga na kituo hicho kwa awamu mbili tofauti ambapo wawili wawili kati yao walishindwa kuondoka nchini mara baada ya kusaini mkataba huo kutokana na kusubiri ruhusa kutoka kwa mwajiri wao.
Akizungumza na East Africa Radio, katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini RT, Suleiman Nyambui amesema, mwanariadha Bazil Baynit na Fabian Naas walijiunga na kituo hicho Jumatatu baada ya kupata ruhusa ambapo Fabian Sulle alijiunga na kituo hicho tangu Mei 17 mwaka huu.
Wanariadha hao ambao bado hawajafikia viwango vya kufuzu kushiriki michuano ya Olimpiki Rio 2016 wanatarajia kuishi katika kambi hiyo hadi Septemba 2016 na katika kipindi hicho watashiriki mashindano mbalimbali ya kufuzu.